KATIBA YA BARAZA LA WAANGALIZI WA
MAKANISA YA KIPENTEKOSTE
(CPCT-MBULU)
SHUKRANI
Shukrani za pekee kwa kamati ya
umoja wa makanisa yote ya kipentekoste  yaliyoshiriki kuandaa  Katiba
hii tarehe 09/04/2015, 31/08/2015, na tarehe 05/09/2015 yaani Makanisa ya Mbulu
Mjini (K.N.Y. Wilaya yote ya Mbulu) kama
ifuatavyo;
(1.) Makanisa ya TAG; Mwangalizi wa makanisa ya TAG (W) Mbulu na
Mwenyekiti wa Umoja huu wa CPCT Mbulu Mchg Isaya Malley, Mchg Paulo P.
Lucas na Mchg Daniel Amnaay.  
(2.) Makanisa ya PAGT;
Mwangalizi wa makanisa ya PAG (W) Mbulu na Makamu Mwenyekiti
wa  Umoja huu wa CPCT Mbulu Mchg Nuhu Mathayo na Mchg Damiano G.
Lazaro
(3.) Makanisa ya VICTORIUS;
Katibu wa Umoja huu wa CPCT MBULU na Mwangalizi wa makanisa ya  VICTORIUS Mchg   Constantine Kifunda.
(4.) Makanisa ya CALVARY;
Mtunza Fedha wa umoja huu wa Mbulu Mchg Marther Ezekiel na Mchg Raheli Ezekiel
na Mwl Basso. 
 (5.) Makanisa ya
FGBF; Mchg Frederick Magafu na Mwangalizi wa Makanisa ya        
       FGBF Mbulu.
(6.) Makanisa ya EAG(T); Mchg
Emanuel Thomas na Mchg Lazaro Emanuel. 
(7.) Makanisa ya FPCT;  Mchg Mathayo Yaato, Mchg Jackob Anton na
MchPaskal Yoram.
(8.) Makanisa ya RGC;
Mchg John S. Machange.
(9.) Makanisa ya GCCT;
 Mchg Emanuel Burra.
Kamati ya
uchapishaji wa Maandishi na uhakiki trh 14-18/09/2015 na 08/10/2015 
1. Mchg Isaya Malley (TAG),
Mwenyekiti wa kamati hii ya uchapishaji CPCT – MBULU
2. Mchg Frederick Magafu (FGBF)
Katibu wa kamati ya uchapishaji CPCT –M BULU. 
3. Mchg Emanuel Thomas (EAG(T)
Mjumbe wa Kamati  CPCT MBULU na
4. Mchg Paulo P. Lucas (TAG)
mjumbe wa Kamati CPCT MBULU.
 UTANGULIZI
Tangu upentekoste uingie Nchini Tanzania
miaka 34 kabla ya uhuru; kumekuwa na muongezeko wa madhehebu ya kipentekoste,
huku kila dhehebu likijitafutia usajiliwa wake binafsi serikalini. Hata hivyo
kwa juhudi kubwa madhehebu ya kipentekoste yalifanya kazi ya kuhubiri injili
 na kutoa huduma za kijamii bila ubaguzi, na kwa jinsi hiyo yakapokeleka
na kufanikiwa kuenea katika jamii ya watanzania.
Sambamba  na mafanikio
iliyoyapata katika kuenea kwake, bado zilijitokeza changamoto za migogoro
miongoni mwao, na kupelekea kuwepo kwa hitaji la kuwa na chombo cha
kuwaunganisha kwa pamoja na kusaidia kutatua migogoro ambayo inajitokeza
miongoni mwao bila kufikishana mahakamani.Mnamo mwaka 1993, chombo hicho
kiliundwa na kujulikana kama baraza la maaskofu  wa makanisa ya
kipentekoste Tanzania ( kwa kiingereza  Pentecostal Council of Tanzania
(PCT), na kwa neema ya Mungu;  mwaka huo huo kikasajiliwa rasmi serikalini.
Miaka 20 baada ya kusajiliwa kwa
PCT, makanisa wanachama yalifanya mkutano wa pamoja, na kuona kuna umuhimu wa
kubadilisha jina la baraza la Maaskofu wa kipentekoste;  Kuwa baraza la
makanisa ya kipentekoste Tanzania;
(BMKT), Kwa kuzingatia uhalisia wa wanachama wake. Mabadiliko haya yalifanyika
pamoja na marekebisho ya katiba ya Baraza, ili kufanikisha utendaji wake.Na
hili ndilo rekebisho la kwanza la katiba ya Baraza ya makanisa ya kipentekoste Tanzania
Na hii imepelekea kuwe na umoja
wa makanisa ya Kipentekoste ya kiwilaya yaani CPCT – MBULU.
YALIYOMO…………………………………………………………(3-4)
1.0.
JINA……………………………………………………..…………5
2.0. MAKAO
MAKUU…………………………………..………...….. 5
3.0. TAMKO LA MAONO
……………………………………….……5 
4.0  MADHUMUNI……………………………………………………..5.
5.0. TAMKO LA
TAFSIRI YA UPENTEKOSTE ………………....…...6
6.0. MAADILI YA
MSINGI (Core values) ………………………....….. 6
7.0. TAMKO LA IMANI
……………………………………………… 7
8.0. UANACHAMA
…………………………………………………… 8
9.0. MUUNDO WA
UONGOZI NA MGAWANYO WA 
        MADARAKA ……………………………………………………..9
10.0 SIFA ZA
VIONGOZI ………………………………………….…12
11.0 JINSI YA
KUWAPATA VIONGOZI WA CPCT - MBULU …....…13
12.0  KUACHA UONGOZI
……………………………………………13  
13.0  IDARA ZA CPTC - MBULU ……………………………………13
13.1 IDARA YA
UINJILISTI NA UMISHENI ………………………...14
13.2 IDARA YA
THEOLOJIA…………………………………………15
13.3 IDARA YA FEDHA,
UCHUMI NA MIPANGO………………... I5
13.4 IDARA YA HUDUMA
ZA JAMII NA MIRADI YA
 MAENDELEO
………………………………………………………..16
 13.5 
IDARA YA ELIMU NA MAFUNZO …………………………..16
13.6 IDARA YA ELIMU
SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARA….16
13.7 IDARA YA
WANAFUNZI NA VYUO VIKUU…………………17
14.0  WAWAKILISHI WA CPCT WA MKOA NA WILAYA
…..........17
15.0 WADHAMINI WA
MALI ZA CPCT ….………………………...17
16.0 MIHURI
…………………………………………..…………... ...18
17.0 MALI YA CPTC ………………………………………………...
.18
18.0 USHAURI WA
KISHERIA …………………………………..….18
19.0 USHIRIKIANO
…………………………………………………. 18
20.0 MIONGOZO
MBALIMBALI YA UTENDAJI ………….......…..18
21.0 MAREKEBISHO YA
KATIBA YA CPCT ………………………18
22.0 ANUANI, EMAIL
NA BLOG YA UMOJA………………………19
1.0  JINA:
Jina la baraza litakuwa ni
 BARAZA LA WAANGALIZI WA
MAKANISA YA KIPENTEKOSTE  MBULU
TANZANIA 
kwa kiingereza ni 
THE COUNCIL OF PENTECOSTAL
CHURCHES OF MBULU IN TANZANIA (CPCT - MBULU).
1.1. NEMBO
Kutakuwa na nembo ya CPCT 
MBULU yenye alama ya msalaba na moto  
a)     
Moto ni ishara ya Roho mtakatifu. Matendo 2:3
b)     
Msalaba ni ishara ya wokovu 1Wakorintho 1:18
2.0. MAKAO MAKUU
Makao makuu kiwilaya yatakuwa
Mbulu Mjini.
 3.0. TAMKO LA MAONO
Kuwa chombo cha kuendeleza,
kudumisha na kulinda umoja  wa roho, imani na ushirika kati ya wanachama
wa CPCT na makundi mengine ya kipentekoste   ulimwenguni kote.
Waefeso  4:3 – 5.
4.0 MADHUMUNI
4.1 Kuwa jumuiya ya kipentekoste
yenye uwezo na uzoefu wa kiroho, na kihuduma, kwa kuleta mabadiliko na mguso
chanya (positive impact) kiroho, kijamii, kiuchumi, kwenye makanisa ya Mungu,
katika Wilaya yetu ya Mbulu na jamii ya kitanzania.
  
4.2. Kuratibu na kusimamia juhudi
za pamoja za kupeleka injili  kwa kutumia vyombo mbalimbali vya
mawasiliano, Mikutano mikubwa ya hadhara, na njia nyinginezo halali kwa kadri
itakavyoonekana inafaa.
4.3. Kutimiza Imani na
mafundisho ya kipentekoste  pamoja na kulinda mambo haya  ili
kusitokee hali ya kurudi nyuma daima tukiongoozwa na Biblia.
4.4 Kuweka na kusimamia utaratibu
wa mahusiano na ushirikiano na mashirika mengine ya kipentekoste Wilayani,
kitaifa na kimataifa.
4.5 Kuendesha mikutano ya pamoja
na maombi, kusifu na kuabudu na Makambi ya umwagiko wa Roho Mtakatifu (camp
meetings) katika ngazi mbalimbali.
4.6 Kumiliki ardhi, majengo, mali
na rasilimali nyinginezo kwa lengo la kuwezesha CPCT kufikia malengo yake.                                                                                                         
4.7. Kuendesha makongamano ya
mafundisho na huduma za kiroho zenye sura ya wilaya kitaifa na kimataifa.
4.8. CPCT katika juhudi za
kutimiza madhumuni na malengo yake itahakikisha inakuwa na ushirikiano na
mashirika, serikali, na vyombo vya umma.
4.9. Kubuni, kuratibu, na
kusimamia miradi itakayosaidia jamii ya Tanzania kujiendeleza katika masuala ya
elimu, afya, maadili mema, maafa, na ustawi katika Nyanja zote za uchumi.
4.10 Kuanzisha au kuendeleza peke
yetu au kwa kushirikiana na mtu yeyote au jumuiya ya watu, miradi mbalimbali,
viwanda, ufundi au jambo linguine ambalo litaonekana kwamba laweza kuendeshwa
bila kuvuruga malengo ya CPCT.
4.11. Kuanzisha kitengo cha
utafiti kwa lengo la kuhakikisha ukuaji wa kanisa  la kikristo  kwa
njia ya umisheni na uinjilisti wa kimkakati na kubadilishana taarifa muhimu.
4.12 Kutoa matamko ya pamoja
yenye lengo la kukemea maovu, maamuzi, nia au matukio 
yoyote yenye mwelekeo wa uvunjifu
wa amani nchini, kuzuia na kuathiri kwa namna yoyote  uhuru wa kuabudu, na
kueneza imani (dini) kama ilivyoainishwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa
Tanzania.
4.13 Kutoa matamko ya
pamoja  yenye lengo na nia ya kuunga mkono maamuzi, kauli, matukio au nia
yenye mwelekeo wa kustawisha jamii ya Tanzania bila kuathiri malengo na imani
ya CPCT.
5.0. TAMKO LA
TAFSIRI YA PENTEKOSTE.
 Ili kuepuka mkanganyo wa uelewa kati ya vyombo
vingine vya kikristo nchini, na kubainisha sifa mama  ya Mpentekoste
asilia, tamko la upekee wa upentekoste  (Distinctive of Pentecostalism )
inaanishwa kama ifuatavyo:
Upentekoste ni imani katika Roho Mtakatifu kwa maeneo yafuatayo
5.1 Kwamba ujazo wa Roho
Mtakatifu ni jambo lililo tofauti na tukio la kuokoka na mtu humpokea Roho
Mtakatifu baada ya kuokoka (the doctrine of subsequences) 
5.2 Kwamba kila ampokeaye Roho
Mtakatifu hunena kwa lugha nyingine kama ishara ya awali ya kujazwa  
Roho Mtakatifu.
5.3 Kwamba ujazo wa Roho
Mtakatifu ni kwa ajili ya utumishi  wa mwamini, na sio kwa ajili ya
utakaso pekee.
5.4 Mpentekoste asili ni yule
ambaye mambo matatu hayo sio imani tu, bali pia yamefanyika maishani mwake, na
anayaishi
6.0  MAADILI YA MSINGI (core values) 
6.1 Uadilifu (intergrity) katika
kila tufanyalo 
  
6.2 Uaminifu wa Biblia kama Neno
la Mungu
6.3 Kicho kwa Roho Mtakatifu na
kazi zake 
6.4 Kusema kweli daima katika
mambo yote.
6.5 Ubora  (excellence)
katika kila tufanyalo.
6.6 Maisha ya ushuhuda mwema na
utakatifu
7.0 TAMKO LA
IMANI 
Tunaamini kuwa:
i.       
Biblia yenye vitabu 66, yaani vitabu 39 Agano la Kale na vitabu 27 katika Agano
Jipya ndio imevuviwa (na sio 72), haina makosa, Neno la Mungu lenye mamlaka la
Mungu. Mithali 30:5-6.
ii.     
Kuna Mungu mmoja, aishiye milele katika nafsi tatu; Baba, Mwana, na Roho
Mtakatifu.
iii.    Uungu wa
Bwana Yesu Kristo, kuzaliwa kwake na bikira, maisha yake yasiyokuwa na dhambi,
miujiza yake, kifo chake cha  kidhabihu na damu yake iokoayo, ufufuko wake
wa mwili, kupaa kwake na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu Baba na kurudi
kwake mara ya pili kwa nguvu na utukufu.
iv.    Wokovu wa
wanadamu waliopotea na kuzaliwa  upya  kufanywako na Roho Mtakatifu
kwa njia ya imani katika Yesu Kristo ni jambo la lazima tukiwa bado tuko
duniani.
v.     
Ubatizo wa Roho Mtakatifu
unaothibitishwa  na kunena kwa lugha mpya kama mtu ajaliwavyo na Roho
Mtakatifu kulingana na Mdo.2:4   utendaji wa karama za Roho
Mtakatifu, na huduma zake.
vi.    Huduma ya Roho Mtakatifu ndani ya mwamini
imwezeshayo kuishi maisha ya uchaji.
vii.  Ufufuo wa wenye haki na wenye dhambi,
Wenye haki ufufuko wa uzima, na wenye dhambi ufufuo wa hukumu.
viii. Kanisa la Yesu Kristo na umoja wa waamini.
ix.    Kuiweka imani ya kikristo kwenye utendaji
wa maisha ya kila siku, na hitaji la kuwahudumia watu katika maeneo yote ya
maisha  ambayo yanajumuisha siyo mambo ya kiroho tu, bali pia, kijamii,
kisiasa na kimwili.       
                                                      
x.     
Agizo kuu la Bwana Yesu,
la kuipeleka injili kamili kwa ulimwengu wote linalojumuisha ubatizo wenye maji
kwa kuzamisha na kuwafanya kuwa wanafunzi wa Yesu. Math 28:18-20.
8.0. UANACHAMA:
8.1.1.Mwanachama wa CPCT atakuwa dhehebu la
kipentekoste litakalokubaliwa na wanachama na mamlaka iliyoidhinishwa na Katiba
hii.
8.1.a.  Maneno “ Dhehebu la
Kipentekoste” au “Dhehebu” katika Katiba hii yana maana ya
shirika          lililosajiliwa
kama kanisa kwa msajili wa vyama vya hiari na masharika yasiyo ya kiserikali,
ambalo imani yake ya utendaji wake kwa mujibu wa tafsiri ya upentekoste na
tamko la imani vilivyoainishwa kwenye Katiba hii, ni la kipentekoste.
8.1.b Huduma ya kipentekoste
isiyo na makanisa inayosimamia, itaruhusiwa kuwa mshirika mwenza (associate
member) lakini siyo mwanachama.
8.2 Sifa za uanachamaKila
dhehebu linalokubaliana na kufuata tamko la imani ya CPCT na mafundisho ya
kipentekoste 
8.3 Wajibu wa wanachama
8.3.1 Kulipa ada ya uanachama.
8.3.2 Kuhudhuria mikutano au
vikao vilivyoainishwa na Katiba hii.
8.3.3 Kushiriki katika kutekeleza
madhumuni ya CPCT
8.4 Haki
za mwanachama zitajumuisha:
8.4.1 Haki za kupiga kura katika
vikao na mikutano ya CPCT.
8.4.2 Haki ya kuchagua na
kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi ndani ya CPCT
8.4.3 Haki ya kutoa mawazo kwenye
mikutano halali na kusikilizwa.
8.4.4 Haki za kupewa huduma
zote  kwa  mujibu miongozo itakayotawala utoaji wa huduma husika.
8.4.5 Wanachama shiriki wana haki
zote isipokokuwa kupiga na kupigiwa kura.
UTARATIBU WA KUJIUNGA NA (CPCT – MBULU)
Utaratibu  wa kujiunga na (CPCT – MBULU)
utafafanuliwa  katika mwongozo.
8.5 Kuacha uanachama
8.5.1 Dhehebu -  mwanachama
ataacha uanachama ikiwa litachagua lenyewe kufanya hivyo na kutoa taarifa kwa
maandishi .
8.5.2  Dhehebu – Mwanachama
litahesabiwa kuwa limepoteza uanachama ikiwa limethibitika kuwa limekengeuka
kiimani, limevunja Katiba ya kanisa lake, limevunja katika ya CPCT limekiuka
maadili ya msingi (core values) ya CPCT kama yalivyoinishwa katika vipengele
6.1. – 6.6
8.5.3  Iwapo Dhehebu –
Mwanachama litakoma kuwepo / kuacha uanachama kwa sababu yoyote ile
halitarudishiwa ada ya usajili, michango yoyote ya fedha au mali, na haki za
uanachama. Pia halitakuwa na haki  ya kuidai  CPCT chochote.
8.5.4 Kutohudhuria vikao vitatu
mfululizo  bila taarifa ya maandishi.
8.5.5 Kushindwa kulipa ada ya
mwaka.
9.0 MUUNDO WA
UONGOZI  NA MGAWANYO WA MADARAKA
9.1.1 Mkutano mkuu
9.1.2 Baraza la Waangalizi au
washauri.
9.1.3 Kamati kuu ya utendaji
 9.1.4  Idara CPCT -
MBULU
9.1.5 Kamati za Wilaya 
MKUTANO MKUU
9.2.1 Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Wilaya watakuwa ni:
-a)      Wajumbe
wote wa kamati wa utendaji wa Wilaya.
b)     
Viongozi watatu wa ngazi  ya juu kutoka kila dhehebu mwanachama. 
c)      
Wadhamini wote wa CPCT – MBULU
d)     
Viongozi wa juu wawili wanachama shiriki kutoka kila kanda (associate members)
e)     
Mwenyekiti na katibu wa  CPCT  kila
Kanda.
f)      
Wakurugenzi wa idara za CPCT  isipokuwa hawatakuwa na haki ya kupiga kura.
9.2.2 Majukumu ya mkutano mkuu
yatakuwa haya
        
i.            Kupokea na
kujadili taarifa na mipango mbalimbali
      
ii.            Kupokea
wanachama wapya
iii.                   
Kuwachagua, kuwatambua na
kuwabariki viongozi wa Wilaya    
              waliochaguliwa na
kuwapa  vyeti.
    
iv.           
Upitishaji bajeti ya kila mwaka.
 v.           
Kuidhinisha idara mpya  za (CPCT – MBULU) zitakazoonekana zitahitajika.
    
vi.            Kufanya
maamuziya mwisho kuhusu mambo ya  ndani ya (CPCT – MBULU)
   
vii.           
Kuidhinisha marekebisho  ya katiba ya (CPCT – MBULU)
 
viii.           
Kuthibitisha  wadhamini
9.3. BARAZA LA
WAANGALIZI NA WASHAURI (CPCT – MBULU) 
Baraza la Waangalizi na washauri
watahudhuria mikutano mikuu yote. Baraza  hili litakutana  mara mbili
kwa mwaka  au zaidi itokeapo mkutano mkuu.
Kutatua migogoro  ndani ya
dhehebu  mwanachama inapokuwa mikubwa  na imeshindikana na
kusuluhishwa ndani ya dhehebu husika.
9.3.1 Wajumbe wake ni hawa
wafuatao 
i.        
Mwenyekiti wa umoja wa wilaya (CPCT – MBULU)
ii.      
Makamu mwenyekiti  (CPCT – MBULU)
iii.     
Katibu mkuu wa Wilaya wa  (CPCT – MBULU)
iv.    
Waangalizi na Wachungaji wa madhehebu  wanachama wa CPCT Wilaya.
9.3.2 mjumbe wa baraza 
la  (CPCT – MBULU) atakoma kuwa mjumbe wa
baraza hilo ikiwa ataacha uongozi (Uchungaji)  kwenye  dhehebu lake
kwa sababu yoyote, au ikiwa dhehebu lake litafutiwa uanachama  wa  (CPCT – MBULU)  kwa mujibu wa katiba
hii.
9.3.2
Majukumu ya baraza la Waangalizi 
i.        
Kusimamia, kutetea, na kulinda imani ya kipentekoste Mbulu. 
ii.     
Kupendekeza majina ya wadhamini wa CPCT
iii.    
Kupitia ripoti  na mipango ya kamati ya utendaji  wa Wilaya kabla
 ya kuwasilisha   
         kwenye mkutako mkuu
iv.      
Kusimamia utekelezaji  wa maazimio ya mkutao mkuu.
v.     Kutoa
misimamo ya pamoja  juu ya maswala ya kijamii Wilayani
vi.    
Kuajiri/ kuwaachisha kazi katibu mkuu na msajili wa  wanachama wapya   
            watakaojiunga na Umoja wetu wa
(CPCT – MBULU)  
vii.      
Kuteua wajumbe wawili wa kamati ya utendaji 
xiii.    
Baraaza hili litakutana mara mbili (2)  kwa mwaka au zaidi
itakapohitajika.
ix.    Kupitisha
miongozo mbalimbali ya idara
9.4 KAMATI YA
UTENDAJI YA KIWILAYA
9.4.1 Kamati ya utendaji ya
Wilaya itakutana mara nne kiwilaya kwa mwaka au zaidi itakapotokea
dharura. Itaundwa na wajumbe wafuatao:-
i.        
Mwenyekiti
ii.      
Makamu mwenyekiti
iii.     
Katibu mkuu
iv.    
Wajumbe wawili na Mhasibu
9.4.2 Majukumu ya kamati ya
Utendaji
i.        
Kusimamia  utekelezaji   wa maazimio ya baraza la Washauri 
na Waangalizi.
ii.      
Kusimamia na kuratibu  vikao  vya Wilaya.
iii.     
Kutayarisha taarifa ya mwaka kwa ajili ya Mkutano mkuu
iv.    
Kusimamia mwenendo wa ofisi za (CPCT – MBULU) Wilaya
v.      
Kusimamia utendaji wa idara za (CPCT – MBULU)
vi.    
Kuandaa agenda za baraza la waangalizi na Mkutano mkuu
vii.    Kuratibu
na kuwa msemaji kwa niaba ya baraza la wqaangalizi katika masuala ya uhusiano
wa ndani na nje.
9.4. Majukumu Ya wajumbe  wa
kamati ya utendaj (CPCT – MBULU)
9.4.1  Majukumu ya
Mwenyekiti (CPCT – MBULU)
i.        
Kuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya kamati kuu ya utendaji, baraza la   Waangalizi na mkutano mkuu (CPCT – MBULU).
ii.      
Kuwa ndiye msemaji wa (CPCT – MBULU) katika mambo yatakayoamiriwa  na
baraza la waangalizi, na mkutano mkuu.
9.4.2 majukumu
ya makamu mwenyekiti
i.        
Kukaimu kazi zote za mwenyekiti wakati mwenyekiti hayupo
ii.       Kufanya
kazi zote anazoagizwa na mwenyekiti.
9.4.3 Majukumu
ya katibu mkuu
i.        
Kuratibu  uendeshaji na utunzaji wa kumbukumbu za mikutano yote ya kamati
kuu ya utendaji, Baraza la Maaskofu, na mkutano mkuu
ii.       Atakuwa
msimamizi mkuu wa ofisi kuu
iii.      Mtendaji wa
kila siku wa shughuli za kamati kuu ya utendaji.
iv.     Kutunza haki zote
muhimu za CPCT pamoja na muhuri wa moto (seal) wa CPCT.
v.       Kuratibu na
kuungansha idara zote za CPCT
vi.     Kuwa mojawapo wa watia
sahihi katika hundi zote za benki na mthibiti mkuu wa   
        
fedha  watakaoajiriwa chini ya ofisi yake.
vii.    Katibu atapatikana kwa
kupendekezwa  na kupigiwa kura na mkutano mkuu na 
          
atafanya kazi kwa mkataba wa miakaka mitatu.
9.4.7 Sifa za
katibu
i.        
Awe mtumishi wa injili aliye na uzoefu wa huduma  isiopungua miaka mitano 
          
katika mji wa Mbulu
ii.       Awe na
elimu ya darasa la saba na kuendelea.
iii.      Awe mwadiliifu,
asiwe na kashfa machoni mwa jamii.
iv.     Awe na uwezo wa
kuwasiliana 
9.4.9 Muda wa
kutumika kwa mjumbe wa kamati ya utendaji
Viongozi hawa watakuwa katika wadhifu huo kwa muda
wa miaka mitatu.Waweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha pili nafasi ya
mwenyekiti itakuwa yamzunguko kwa muda wa miaka mitatu kwa kila dhehebu
mwanachama.
9.4.10. TARATIBU ZA KUENDESHA
VIKAO
i.        
Vikao vyote vya (CPCT) vitafanyika kwa namna ambavyo imeelezwa nadani ya
katiba  ya CPCT. Kikao ambacho hakitafuata utaratibu uliotajwa ndani ya
katiba  ya CPCT kitakuwa batili.
ii.       Vikao
halali vya CPCT vitakuwa na wajumbe  wasiopungua theluthi mbili (2/3)
 ya wajumbe wa ngazi husika  (kwa kikao chochote  ndani ya 
CPCT)
iii.      Maamuzi ya
vikao  vyote vya CPCT vitakuwa ni theluthi mbili (2/3) ya wajumbe wa
mkutano husika.
10.0 SIFA ZA VIONGOZI
Kukubaliana na sifa zote  za kibiblia na kuwa
:-
10.1 Mtu ambaye amezaliwa mara ya pili
10.2 Mtu abaye amejazwa roho mtakatifu 
10.3 Mume wa mke  mmoja 
10.4 Mwenye vipawa na uwezo wa uongozi 
10.5 Ni lazima awe na ushuhuda mzuri  
10.6  Mtu mwenye elimu ya kusoma na kuandika
10.7 Awe na uwezo  wa kuwasiliana 
11.0. JINSI YA KUWAPATA
VIONGOZI WA  CPCT
11.1 Viongozi wa CPCT watapatikana kutokana na
uchaguzi utakaofanyika katika mkutano mkuu wa mwaka  wa uchaguzi, kila
baada ya miaaka miatatu. Mwenyekiti na makamu mwenyekiti  wa CPCT taifa
watachaguliwa katika mkutano mkuu  wa uchaguzi  kutoka miongoni mwa
viongozi wachungaji wa dhehebu na wanachama kwa ajili ya kupigiwa kura. 
11.2 Viongozi watachaguliwa kila wiki ya wiki ya
kwanza ya mwezi wa sita mwaka  wa uchaguzi. Makabidhiano  ya kiofisi
yatafanyika ndani ya siku thelathini (30) baada ya uchaguzi.
11.3 Wiongozi waliochaguliwa watakauwa madarakani
kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane ya mwaka wa uchaguzi hadi tarehe 30 mwezi wa
saba ya mwaka mwingine wa uchaguzi
11.4 Wakati wa uchaguzi wa kiwilaya, koramu ya
wajumbe lazima ifikie ziada ya asilimia hamsini ya wanachama hai (kwa kulipa
ada) zote na mchango kwa bajeti ya CPCT  Wilaya) na pia kigezo cha
aliyechaguliwa kitakuwa ni theluthi mbili ya kuwapiga kura iwe ya siri kwa
wote.
11.5 utratibu huu utatumika kwa chaguzi za kamati
ya utendaji Wilaya, tarafa na kata.
12.0 KUACHA UONGOZI
 Kiongozi yeyote wa CPCT itambidi aache
uongozi kkufuatia mojawapo  ya hali hizi zifuatazo  ikitokea:
12.1 kumalizika kwa muda wa kushika uongozi 
12.2 kuacha uongozi kwa hiari ya kiongozi mwenyewe
akiwa ametoa taarifa ya miezi mitatu kwa maandishi kuhusu jambo hilo  kwa
mamlaka iliyomchagua ya CPCT
12.3 Wakati ule atakapoacha kuwa mwakilishi wa
dhehebu lake.
12.4 Wakati atakapothibitishwa na Baraza la
waangalizi kwamba amekiuka katiba na tamko la imani ya  CPCT
12.5 Atakapokuwa ameshindwa kuhudhuria vikao vya
kawaida vya  CPCT vitatu mfululizo bila ya kuwa na sababu za maana 
zenye kuridhisha.
13.0 IDARA ZA CPCT - MBULU
Baraza la maaskofu baada ya ushauri wa kamati ya
utendaji kubadilika itaanzisha idara yeyote ile kwa kusudi la kurahisisha 
utendaji wa kazi  za CPCT kama ifuatavyo;
a)      Uinjilisti na
umisheni
b)      Idara ya
thiologia
c)      
Mambo ya kimataifa na mahusiano (Mf. compassion, world vision nk)
  
d)      Habari za
utangazaji na uchapaji (Mfano kutoa habari za umoja wetu kwenye 
        
magazeti, blogs, mahojiano ya Radio, kotoa vijarida vinavyoelezea
maendeleo 
        
au mafanikio ya umoja huu, Television nk
e)      Fedha uchumi, na
mipango
f)       Huduma za
jamii na miradi ya maendeleo
g)      Idara za vijana
(mashuleni, vyouni, na vyuo vikuu)
h)      Idara ya
wanawake 
i)       
Idara ya elimu na mafunzo 
(Mfano kuandaa semina mbalimbali au
kuwatoa baadhi ya wajumbe kwenye umoja wetu kwenda kuwasomesha kwa ajili ya
kuendesha miradi mipya ambayo itatokana na umoja wetu).
13.1 IDARA YA UINJILISTI NA
UMISHENI
14.1 idara hii itakuwepo kwa kusaidia na kuratibu
na kusimamia upelekaji wa innjili kwa njia ya mikutano mikubwa ya hadhara,
kubuni na kuhamasisha mbinu mbalimbali za uinjilisti wa ushirikiano wa
madhehebu  wanachama. Pia itaratibu na kushauri juhudi za dhehebu
lolote  mwanachama lililo na mipango ya kufanya umisheni ndani na nje ya
nchi ikiwa n pamoja na kulitafutia vitendea kazi kwa bei nafuu.
14.2 Viongozi wa idara hii watakuwa:-
Mkurungenzi mkuu atakayekuwa mwenyekiti wa vikao
vyote na kiongozi mkuu.
14.3 naibu mkurungenzi mkuu atakayemsaidia
mwenyekiti katika shughuli zake na kukaimu uenyekiti anapokuwa hayupo.
14.4 Katibu ndiye atakayekuwa mtendaji mkuu wa
maamuzi yote ya kamati, na wajumbe wanne.
14.5 sifa za viongozi zitakuwa Kama ifuatavyo:-
i.        
Mwenyekiti awe mtumishi wa injili mwenye uzoefu wa kuratibu mikutano 
mikubwa ya injili  kwa muda usiopungua miaka mitano.
ii.      Atokane na moja
ya dhehebu mwanachama.
Wajumbe wanaweza kuwa washiriki au watumishi wa
madhehebu wanachama wanaojulikana kuwa na uzoefu katika huduma ya uinjilisti,
mwenye mzigo na uzoefu wa mikutano ya injili.
13.2  IDARA YA
THEOLOJIA 
13.1 Idara hii itakuwepo na makusudi ya kulinda
imani na kuitetea dhidi ya upotofu unaweza kuathiri au kutoa taswira
mbaya  ya upentekoste, kubuni, kuraitibu na kuwezesha utoaji elimu ya
biblia na theologia  yenye malengo au mkazo wa kipentekoste, na kutoa mafunzo
mbalimbali kwa lengo la kuharakishwa utimizaji wa malengo ya CPCT. Idara hii
itaratibu na kuandaa makongamano ya kiwilaya na kitaifa ya mafundisho ya kiroho
na uamsho ya kipentekeste yatakayoshirikisha madhehebu wanachama wote.
13.2 Vongozi wa idara hii watakuwa:-
i.        
Mkurugenzi mkuu ambaya atakuwa mwenyekiti na kiongozi mkuu
ii.       Naibu
mkurungezi mkuu atakayemsaidia mwenyekiti
iii.      Katibu mkuu
atakayekuwa mtendaji mkuu wa maamuzi ya kamati, na wajumbe watano
kutoka kwenye madhebu wanachama. Mkurungezi mkuu atatakiwa kuwa na sifa
zifuatazo:-
-         
Awe mtumishi wa injili mwenye uzoefu katika huduma usiopugua miaka kumi.
-         
Awe na uwezo wa kufundisha, kutetea na kujenga hoja.
-         
Awe madilifu, asiye na kashfa mbele ya jamii
Naibu wake, na katibu watakuwa na sifa
zifuatazo:-
Wawe na elimu au zaidi pamoja na sifa nyingine
kama za mkurungenzi mkuu. Wajumbe wengine wa kamati  wawe watumishi wenye
uzoefu katika huduma ya injili isiopungua miaka mitano.
13.3. IDARA YA FEDHA, UCHUMI NA
MIPANGO
 Majukumu
yake yatamjulisha:-
i.        
Kuratibu maandalizii na uundaji wa sera na mipango mikakati ya CPCT
ikishirikiana na baraza la waangalizi/washauri
ii.       Kukagua na
kutolea taarifa  na ushauri utekelezaji wa sere na mipangoo mikakati,
mipango maalum kwa baraza la waangalizi/washauri.
iii.      Kushauri baraza
la waangalizi na idara nyingine za CPCT katika masuala ya kiushumi na uandaaji
bajeti zake.
iv.     Kutoa ushauri kwa
wanachama wa CPCT katka mambo yahusuyo mipambo, na maendeleo yafaayo wakati
utakapohitajika.
13.3.1 Idara
hii itaundwa na bodi yenye wajumbe wafuatao:-     
i.        
Mkurugenzi mkuu. Huyu atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya bodi, na kiungo
katika bodi ya baraza la waangalizi
ii.       Makamu
mwenyekiti. Huyu atakuwa mshauri wa mwenyekiti na kufanya kazi zake anapokuwa
hayupo na amekasimu madaraka kwa makamu.
iii.      Mratibu mkuu.
Atachukua na kutunza miniti za vikao vya bodi, na msimamizi mkuu wa vitengo vya
bodi.
 13.3.2 Bodi itakuwa
na vitengo vivuatavyo:-
      Kitengo mpango mkakati;    Kitengo hiki kitahusika na uandaaji  wa mpango mkakati na usimamizi wa
mchakato wake wote. Kitaundwa na wajumbe kumi  wenye taaluma ya mipango.
Katika wajumbe hao kumi watatu lazima wawe wachungaji.
Sifa za wajumbe hao ni:-
i.        
Wawe washirika au wachungaji watokanao na madhehebu wanachama
ii.       Wawe na
stashahada ya kwanza au zaidi ya mipango mingine yoyote inayojumuisha elimu
 ya mipango na utawala.
13.3.3  Kitengo cha uchumi na fedha
Kitengo hiki kitahusika  mipango  ya
mambo ya uchumi, upatikanaji na uwezeshaji mali na fedha , na usimamizi au
ukaguzi wa mahesabu (accounting and auditing) na maandalizi ya bajeti  ya
baraza la waangalizi la CPCT ya mara kwa mara. Kitengo hiki kitaundwa na
wataalum wafuatao wa fedha:-
i.        
Mkurugenzi makamu wake utawala (managing 
director) atakayesimamia vikao na utendaji wa kitengo
ii.       Mtunza
mahesabu mkuu (chief accountant ) atakayesimamia timu ya utawala wa mwendo wa
mahesabu ya fedha CPCT.
iii.      Mtunza
maahesabu utawala  (management accountant) atakayesimamia na kutoa taarifa
ya halali ya fedha kwa utawala wa ndani (management accounting) wa CPCT 
Hawa, pamoja na kazi nyingine watakazofanya
kulingana na majukumu yao kama yalivyoaininshwa hapo juu, watakuwa na vikao vya
pamoja vitakavyoandaa mipango ya uchumi na bajeti za CPCT  kwa kuzingatia
taratibu rejea zitakazoagizwa na baraza la wangalizi kwa marrekebisho/maridhio.
13.4 IDARA ZA HUDUMA ZA JAMII NA
MIRADI YA MAENDELEO 
Idara hii itakuwepo kwa kusudi la kubuni na
kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na maafa  kama elimu, Afya
  huduma za kifedha, ufundi stadi, biashara, utoaji misaada kwa
waliopata majanga ya mafuriko, moto au mengineyo, idara hii pia itashirikiana
na idara ya utendaji  ya CPCT  itatafuta fedha nje na ndani ya nchi
kwa kusudi lakufikia malengo yake 
13.5. IDARA YA ELIMU NA
MAFUNZO 
Majukumu yake yatajumuisha
i.        
Kuchambua kwa kina na kuwezesha kupata nafasi za mafunzo kwaajili ya watumishi
wa Mungu walio  chini ya wanachama wa CPCT
ii.       Kupanga
kuendsha na kuunganisha mambo yahusuyo mafunzo ya muda mfupi  na semina
hapa nchini
iii.      Kuchambua kwa
makini watoa misaada na kuwatuma watumishi wa mungu  na wakristo nchi za
nje wapate mafunzo
iv.     Kuanzisha mashule,
 vyuo na vyuo vikuu kwa ajili ya  kufundisha  wakristo na
watumishi wa Mungu
v.       Atawajibika
kwa Katibu Mkuu
13.6. IDARA YA WANAFUNZI WA
SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
13.6.1 Idara hii itakuwepo  kwa kusudi la
kuratibu upelekaji wa huduma za kiroho kwa wanafunzi katika shule za msingi, na
sekondari kwa watoto watokao kwenye makanisa ya kipentekoste. Kwa kuunganisha
juhudi za pamoja za madhehebu wanachama, idara hii itaratibu utoaji wa mafundisho
na huduma kwa wanafunzi wilaya yote.
13.6.2
Viongozi wa idara hii watakuwa ni:
i.        
Mkurugenzi mkuu atakayekuwa mwenyekiti na kiongozi mkuu wa idara.
ii.       Naibu
mkuruugenzi mkuu atakayemsaidia mwenyekiti  
iii.      Katibu mkuu
atakayekuwa mtendaji mkuu wa maamuzi ya uongozi.
13.6.3 Sifa za viongozi hawa
zitakuwa kama ifuatavyo:-
i.       Atakuwa mtumishi wa injili mwenye wito na
wanafunzi ili atoe muda kwa kazi hiyo.
ii.       Awe na
elimu ya theologian a kutumikia miaka zaidi ya tano 
iii.      Asiwe na kashfa
machoni pa jamii
13.6.4 Makamu mkurugenzi – awe na sifa zote za
mkurugenzi mkuu. Katibu mkuu awe na sifa  
          
za mkurugenzi mkuu isipokuwa halazimiki 
13.7 IDARA YA WANAFUNZI WA VYUO
NA VYUO VIKUU
i.        
Idara hii itakuwepo kwa kusudi la kuratibu utoaji huduma za kiroho kwa
wanafunzi wa vyuo vikuu watkao kwenyye makanisa ya kipentekoste nchini   
i.      
Viongozi  wa idara hii watakuwa na sifa kama viongozi wa idara ya viongozi
wa idara ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ispokuwa sifa ya elimu za
viongozi. Viongozi wa idara hii watapaswa kuwa na elimu ya theolojia ya shahada
moja au nyingine 
iii.      Idara hii
itakuwa na mwongozo wake utakao fafanua utendaji kazi wake.
14.0 WAWAKILISHI WA CPCT WA
MKOA, WILAYA, TARAFA AU KATA
14.1 kutakuwepo na wawakilishi wa CPCT kayika
mikoa na wilaya za Tanzania. Chaguzi la wawakilishi wa CPCT ngazi ya mkoa na
wilaya zitafanyika mwezi wa tisa baada ya viongozi wapya kuingia madarakani.
14.2. utaratibu wa kuundwa kwa ofisi za mikoa na
wilaya kutafafanuliwa  katika  mwongozo wa utendaji ambao 
utaandaliwa kuwa mujibu wa katiba hii.
14.3 sifa za wawakilishi, muda wao wa kushika
nafasi hizo na kuacha kazi kwao vitakuwa sawa na ilivyo kwa ajili ya nafasi
nyingiinezo za uongozi ndani CPCT
15.0 WADHAMINI WA MALI ZA
CPCT 
15.1 wadhamini
15.2. CPCT itakuwa na wadhamini saba
watakaosajiliwa kisheria.
15.3. wadhamini hao watajumuisha watu saba
wafuatao:-
i.        
Mwenyekiti wa CPCT 
ii.       Katibu
mkuu wa CPCT 
iii.      Wajumbe watano
watakaokuwa mamechaguliwa miongom=ni mwa baraza la waangalizi
15.3.1 wadhamini watamchagua mwenyekiti wao ambaye
ndiiye atakuwa mdhamini mtendaji na mtunza mihuri
15.3.2 wadhamini watawajibika kutunza mali zote
 za CPCT zinazohamishika zikijumlishwa na ardhi  na vilivyo ndani
yake, majengo, mashine, magari na mali yoyoite ile ambayo inapatikana kwa jina
la CPCT.
15.3.3 wadhamini watashika wadhifa huo kwa miaka
mitatu mfululizo lakini waweza kuchaguliwa kwa muda wa miaka mitatu mingine.
15.3.4 mdhamini yeyote ataacha kuwa mdhamini kwa:-
i.        
Mda wa wadhifa wake utakapoisha
ii.       Yeye
mwenyewe kwa hiari yake  kutoa taarifa mapema kwa mkutano mradi tu awe
hana deni na CPCT                   
                                                                                      
 iii.     
Sababu kuna ushahidi wa kuaminika kwamba mdhamini Yule ni mbinafsi na kwamba
ametumia mali ya CPCT kwa faida yake binafsi.
iv.     Dhehebu atokalo
likikoma uanachama
v.       Uongozi
wake ukikoma katika dhehebu lake
vi.     Akifariki
16.0 MIHURI
Kutakuwa na mihuri ya aina mbili
i.        
Mhuri wa chuma   
ii.      
Mhuri wa kawaida
Wadhamini watautunza mhuri wa CPCT mahali pa
usalama na kuhakikisha kuwa unatumika  kihalali. Uwekaji wa mhuri wa CPCT
katika hati yoyote itabidi ufanywe na wadhamini wa CPCT  wasiopungua
watatu, mmojawapo lazima awe mwenyekiti au katibu mkuu au mmoja wa wadhamini.
17.0 MALI YA CPCT.
17.1 CPCT  MBULU itajipatia mali yake yenyewe
na kuimiliki kwa kuipata katika sehemu yeyote nchini au nje ya Tanzania kwa
ajili ya matumizi yake  na itahiari kuiondoa mali yake baada ya kupata
kibali cha mkutano mkuu   wa CPCT
17.2 mali yote Ya CPCT  itatunzwa na
kutawaliwa  na wadhamini ambao watakuwa wamechaguliwa na chombo
kinachohusika  cha CPCT 
17.3 Mwanachama yayote wa CPCT  ambaye
ataacha kuwa mwanachama kwa sababu  iwayo yoyote ili hatadai kulipwa
sehemu yoyote ya mali ya CPCT 
18.0 USHAURI WA KISHERIA
CPCT itatafuta ushauri  wa kisheria, katika
mambo ya mikataba, matamko na mambo mbalimbali yahusuyo sheria.
19.0 USHIRIKIANO
CPCT – MBULU inatambua na itajiunga na mashirika
mengine ya kipentekoste ya Wilaya na kitaifa kwa kusudi la kujenga ushirika wa
kiroho, na kuunganisha nguvu za kihuduma kwa kuanzia hapa inatamkwa wazi kuwa
CPCT itajiunga rasmi kuwa mwanachama wa pentekoste world fellowship (PWF)
ambalo tamko lake la imani imekubali kuwa tamko lake pia.
20.0. MIONGOZO MBALIMBALI YA
UTENDAJI
20.1 kwa mujibu wa katiba hii, pia kutakuwepo na
miongozo ya utendaji ambayo itaweka utaratibu na kanuni mbalimbali
zitakazosaidia kuendesha  CPCT ili mradi miongozo hiyo haikiuki sheria
zilizomo ndani ya katiba hii.                                                         
             
20.2 Ni lazima miongozo yote iwe na sahihi ya
mwenyekiti wa baraza la waangalizi na katibu.
20.3 kila idara itaundwa mwongozo wa idara yake
utakapopitishwa na baraza la Waangalizi ikishirikiana na wataalum wa mambo ya
sheria.
21.0 MAREKEBISHO YA KATIBA YA
CPCT
Mkutano mkuu unaweza kurekebisha katiba mradi:
21.1 taarifa ya maandishi ya miezi mine kabla ya
mkutano mkuu iwe imetolewa na mwanachama yeyote kwa katibu mkuu kabla ya kikao
cha mkutano mkuu akionyesha kusudi lake la kutaka katiba  irekebishwe
atajaza wap na kifungu kipi na vifungu vipi virekebishwe an kwa sababu
zipi  anapendekeza marekebisho.
21.2 kamati kuu itatoa maandishi  miezi
miwili kwa wanachama wa CPCT  kabla mkutano mkuu haujakaa ikionyesha
kusudi la kurekebisha katiba kwa kuta wazi ni kifungu  au vifungu vipi
inapendekeza virekebishe
21.3. Mkutano mkuu utakaorekebisha katiba
utahitaji kuhudhuriwa na 50% ya wanachama wote wa CPCT na katika  
hao watakaohudhuria wawe wamepiga kura  ya kukubali mapendekezo ya
kirekebisha katiba.
Imetolewa na :
Baraza la
Makanisa ya Kipentekoste (CPCT – Mbulu), Manyara, Tanzania au
Council of
Pentecostal Churches of Mbulu in Tanzania (CPCT) 
22.0 ANUANI, EMAIL NA BLOG YA
BARAZA LA WAANGALIZI LA 
UMOJA WA MAKANISA YA
KIPENTEKOSTE MBULU
SLP 103,
MBULU, MANAYARA – TANZANIA
Simu / +255
784 890 972; +255 784 478 177,
Blog ya umoja wa CPCT Mbulu;  cpctmbulu.blogspot.com