Alhamisi, 31 Desemba 2015

MUNGU IBARIKI TANZANIA 2016 UWE MWAKA WA BARAKA NA MAFANIKIO


Mungu mbariki Rais wetu Dr Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri mkuu Mheshimiwa Ndg Majaliwa, Baraza la mawaziri, Bunge la Tanzania, Wakuu wa mikoa, Wilaya nk

Mungu Bariki wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao

Ijumaa, 9 Oktoba 2015

NEW CPCT MBULU CONSTITUTION



KATIBA YA BARAZA LA WAANGALIZI WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE (CPCT-MBULU)
SHUKRANI

Shukrani za pekee kwa kamati ya umoja wa makanisa yote ya kipentekoste  yaliyoshiriki kuandaa  Katiba hii tarehe 09/04/2015, 31/08/2015, na tarehe 05/09/2015 yaani Makanisa ya Mbulu Mjini (K.N.Y. Wilaya yote ya Mbulu) kama ifuatavyo;

(1.) Makanisa ya TAG; Mwangalizi wa makanisa ya TAG (W) Mbulu na Mwenyekiti wa Umoja huu wa CPCT Mbulu Mchg Isaya Malley, Mchg Paulo P. Lucas na Mchg Daniel Amnaay.  

(2.) Makanisa ya PAGT; Mwangalizi wa makanisa ya PAG (W) Mbulu na Makamu Mwenyekiti wa  Umoja huu wa CPCT Mbulu Mchg Nuhu Mathayo na Mchg Damiano G. Lazaro

(3.) Makanisa ya VICTORIUS; Katibu wa Umoja huu wa CPCT MBULU na Mwangalizi wa makanisa ya  VICTORIUS Mchg   Constantine Kifunda.

(4.) Makanisa ya CALVARY; Mtunza Fedha wa umoja huu wa Mbulu Mchg Marther Ezekiel na Mchg Raheli Ezekiel na Mwl Basso. 

 (5.) Makanisa ya FGBF; Mchg Frederick Magafu na Mwangalizi wa Makanisa ya       
       FGBF Mbulu.

(6.) Makanisa ya EAG(T); Mchg Emanuel Thomas na Mchg Lazaro Emanuel. 

(7.) Makanisa ya FPCT;  Mchg Mathayo Yaato, Mchg Jackob Anton na MchPaskal Yoram.

(8.) Makanisa ya RGC; Mchg John S. Machange.

(9.) Makanisa ya GCCT;  Mchg Emanuel Burra.

Kamati ya uchapishaji wa Maandishi na uhakiki trh 14-18/09/2015 na 08/10/2015 

1. Mchg Isaya Malley (TAG), Mwenyekiti wa kamati hii ya uchapishaji CPCT – MBULU
2. Mchg Frederick Magafu (FGBF) Katibu wa kamati ya uchapishaji CPCT –M BULU. 
3. Mchg Emanuel Thomas (EAG(T) Mjumbe wa Kamati  CPCT MBULU na
4. Mchg Paulo P. Lucas (TAG) mjumbe wa Kamati CPCT MBULU.


 UTANGULIZI

Tangu upentekoste uingie Nchini Tanzania miaka 34 kabla ya uhuru; kumekuwa na muongezeko wa madhehebu ya kipentekoste, huku kila dhehebu likijitafutia usajiliwa wake binafsi serikalini. Hata hivyo kwa juhudi kubwa madhehebu ya kipentekoste yalifanya kazi ya kuhubiri injili  na kutoa huduma za kijamii bila ubaguzi, na kwa jinsi hiyo yakapokeleka na kufanikiwa kuenea katika jamii ya watanzania.

Sambamba  na mafanikio iliyoyapata katika kuenea kwake, bado zilijitokeza changamoto za migogoro miongoni mwao, na kupelekea kuwepo kwa hitaji la kuwa na chombo cha kuwaunganisha kwa pamoja na kusaidia kutatua migogoro ambayo inajitokeza miongoni mwao bila kufikishana mahakamani.Mnamo mwaka 1993, chombo hicho kiliundwa na kujulikana kama baraza la maaskofu  wa makanisa ya kipentekoste Tanzania ( kwa kiingereza  Pentecostal Council of Tanzania (PCT), na kwa neema ya Mungu;  mwaka huo huo kikasajiliwa rasmi serikalini.

Miaka 20 baada ya kusajiliwa kwa PCT, makanisa wanachama yalifanya mkutano wa pamoja, na kuona kuna umuhimu wa kubadilisha jina la baraza la Maaskofu wa kipentekoste;  Kuwa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania; (BMKT), Kwa kuzingatia uhalisia wa wanachama wake. Mabadiliko haya yalifanyika pamoja na marekebisho ya katiba ya Baraza, ili kufanikisha utendaji wake.Na hili ndilo rekebisho la kwanza la katiba ya Baraza ya makanisa ya kipentekoste Tanzania
Na hii imepelekea kuwe na umoja wa makanisa ya Kipentekoste ya kiwilaya yaani CPCT – MBULU.

YALIYOMO…………………………………………………………(3-4)

1.0. JINA……………………………………………………..…………5

2.0. MAKAO MAKUU…………………………………..………...….. 5

3.0. TAMKO LA MAONO ……………………………………….……5 

4.0  MADHUMUNI……………………………………………………..5.

5.0. TAMKO LA TAFSIRI YA UPENTEKOSTE ………………....…...6

6.0. MAADILI YA MSINGI (Core values) ………………………....….. 6

7.0. TAMKO LA IMANI ……………………………………………… 7

8.0. UANACHAMA …………………………………………………… 8

9.0. MUUNDO WA UONGOZI NA MGAWANYO WA
        MADARAKA ……………………………………………………..9

10.0 SIFA ZA VIONGOZI ………………………………………….…12

11.0 JINSI YA KUWAPATA VIONGOZI WA CPCT - MBULU …....…13

12.0  KUACHA UONGOZI ……………………………………………13  

13.0  IDARA ZA CPTC - MBULU ……………………………………13

13.1 IDARA YA UINJILISTI NA UMISHENI ………………………...14

13.2 IDARA YA THEOLOJIA…………………………………………15

13.3 IDARA YA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO………………... I5

13.4 IDARA YA HUDUMA ZA JAMII NA MIRADI YA
 MAENDELEO ……………………………………………………..16

 13.5  IDARA YA ELIMU NA MAFUNZO …………………………..16

13.6 IDARA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARA….16

13.7 IDARA YA WANAFUNZI NA VYUO VIKUU…………………17

14.0  WAWAKILISHI WA CPCT WA MKOA NA WILAYA …..........17

15.0 WADHAMINI WA MALI ZA CPCT ….………………………...17

16.0 MIHURI …………………………………………..…………... ...18

17.0 MALI YA CPTC ………………………………………………... .18

18.0 USHAURI WA KISHERIA …………………………………..….18

19.0 USHIRIKIANO …………………………………………………. 18

20.0 MIONGOZO MBALIMBALI YA UTENDAJI ………….......…..18

21.0 MAREKEBISHO YA KATIBA YA CPCT ………………………18

22.0 ANUANI, EMAIL NA BLOG YA UMOJA………………………19

1.0  JINA:

Jina la baraza litakuwa ni
 BARAZA LA WAANGALIZI WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE  MBULU TANZANIA 

kwa kiingereza ni 
THE COUNCIL OF PENTECOSTAL CHURCHES OF MBULU IN TANZANIA (CPCT - MBULU).

1.1. NEMBO

Kutakuwa na nembo ya CPCT  MBULU yenye alama ya msalaba na moto  

a)      Moto ni ishara ya Roho mtakatifu. Matendo 2:3

b)      Msalaba ni ishara ya wokovu 1Wakorintho 1:18

2.0. MAKAO MAKUU

Makao makuu kiwilaya yatakuwa Mbulu Mjini.

 3.0. TAMKO LA MAONO

Kuwa chombo cha kuendeleza, kudumisha na kulinda umoja  wa roho, imani na ushirika kati ya wanachama wa CPCT na makundi mengine ya kipentekoste   ulimwenguni kote. Waefeso  4:3 – 5.

4.0 MADHUMUNI

4.1 Kuwa jumuiya ya kipentekoste yenye uwezo na uzoefu wa kiroho, na kihuduma, kwa kuleta mabadiliko na mguso chanya (positive impact) kiroho, kijamii, kiuchumi, kwenye makanisa ya Mungu, katika Wilaya yetu ya Mbulu na jamii ya kitanzania.
 
4.2. Kuratibu na kusimamia juhudi za pamoja za kupeleka injili  kwa kutumia vyombo mbalimbali vya mawasiliano, Mikutano mikubwa ya hadhara, na njia nyinginezo halali kwa kadri itakavyoonekana inafaa.

4.3. Kutimiza Imani na mafundisho ya kipentekoste  pamoja na kulinda mambo haya  ili kusitokee hali ya kurudi nyuma daima tukiongoozwa na Biblia.

4.4 Kuweka na kusimamia utaratibu wa mahusiano na ushirikiano na mashirika mengine ya kipentekoste Wilayani, kitaifa na kimataifa.

4.5 Kuendesha mikutano ya pamoja na maombi, kusifu na kuabudu na Makambi ya umwagiko wa Roho Mtakatifu (camp meetings) katika ngazi mbalimbali.

4.6 Kumiliki ardhi, majengo, mali na rasilimali nyinginezo kwa lengo la kuwezesha CPCT kufikia malengo yake.                                                                                                          4.7. Kuendesha makongamano ya mafundisho na huduma za kiroho zenye sura ya wilaya kitaifa na kimataifa.

4.8. CPCT katika juhudi za kutimiza madhumuni na malengo yake itahakikisha inakuwa na ushirikiano na mashirika, serikali, na vyombo vya umma.

4.9. Kubuni, kuratibu, na kusimamia miradi itakayosaidia jamii ya Tanzania kujiendeleza katika masuala ya elimu, afya, maadili mema, maafa, na ustawi katika Nyanja zote za uchumi.

4.10 Kuanzisha au kuendeleza peke yetu au kwa kushirikiana na mtu yeyote au jumuiya ya watu, miradi mbalimbali, viwanda, ufundi au jambo linguine ambalo litaonekana kwamba laweza kuendeshwa bila kuvuruga malengo ya CPCT.

4.11. Kuanzisha kitengo cha utafiti kwa lengo la kuhakikisha ukuaji wa kanisa  la kikristo  kwa njia ya umisheni na uinjilisti wa kimkakati na kubadilishana taarifa muhimu.

4.12 Kutoa matamko ya pamoja yenye lengo la kukemea maovu, maamuzi, nia au matukio
yoyote yenye mwelekeo wa uvunjifu wa amani nchini, kuzuia na kuathiri kwa namna yoyote  uhuru wa kuabudu, na kueneza imani (dini) kama ilivyoainishwa na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

4.13 Kutoa matamko ya pamoja  yenye lengo na nia ya kuunga mkono maamuzi, kauli, matukio au nia yenye mwelekeo wa kustawisha jamii ya Tanzania bila kuathiri malengo na imani ya CPCT.

5.0. TAMKO LA TAFSIRI YA PENTEKOSTE.

 Ili kuepuka mkanganyo wa uelewa kati ya vyombo vingine vya kikristo nchini, na kubainisha sifa mama  ya Mpentekoste asilia, tamko la upekee wa upentekoste  (Distinctive of Pentecostalism ) inaanishwa kama ifuatavyo:

Upentekoste ni imani katika Roho Mtakatifu kwa maeneo yafuatayo

5.1 Kwamba ujazo wa Roho Mtakatifu ni jambo lililo tofauti na tukio la kuokoka na mtu humpokea Roho Mtakatifu baada ya kuokoka (the doctrine of subsequences) 

5.2 Kwamba kila ampokeaye Roho Mtakatifu hunena kwa lugha nyingine kama ishara ya awali ya kujazwa   Roho Mtakatifu.

5.3 Kwamba ujazo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya utumishi  wa mwamini, na sio kwa ajili ya utakaso pekee.

5.4 Mpentekoste asili ni yule ambaye mambo matatu hayo sio imani tu, bali pia yamefanyika maishani mwake, na anayaishi

6.0  MAADILI YA MSINGI (core values) 

6.1 Uadilifu (intergrity) katika kila tufanyalo 
 
6.2 Uaminifu wa Biblia kama Neno la Mungu

6.3 Kicho kwa Roho Mtakatifu na kazi zake 

6.4 Kusema kweli daima katika mambo yote.

6.5 Ubora  (excellence) katika kila tufanyalo.

6.6 Maisha ya ushuhuda mwema na utakatifu

7.0 TAMKO LA IMANI 

Tunaamini kuwa:

i.        Biblia yenye vitabu 66, yaani vitabu 39 Agano la Kale na vitabu 27 katika Agano Jipya ndio imevuviwa (na sio 72), haina makosa, Neno la Mungu lenye mamlaka la Mungu. Mithali 30:5-6.

ii.      Kuna Mungu mmoja, aishiye milele katika nafsi tatu; Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.

iii.    Uungu wa Bwana Yesu Kristo, kuzaliwa kwake na bikira, maisha yake yasiyokuwa na dhambi, miujiza yake, kifo chake cha  kidhabihu na damu yake iokoayo, ufufuko wake wa mwili, kupaa kwake na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu Baba na kurudi kwake mara ya pili kwa nguvu na utukufu.

iv.    Wokovu wa wanadamu waliopotea na kuzaliwa  upya  kufanywako na Roho Mtakatifu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo ni jambo la lazima tukiwa bado tuko duniani.

v.      Ubatizo wa Roho Mtakatifu unaothibitishwa  na kunena kwa lugha mpya kama mtu ajaliwavyo na Roho Mtakatifu kulingana na Mdo.2:4   utendaji wa karama za Roho Mtakatifu, na huduma zake.

vi.    Huduma ya Roho Mtakatifu ndani ya mwamini imwezeshayo kuishi maisha ya uchaji.

vii.  Ufufuo wa wenye haki na wenye dhambi, Wenye haki ufufuko wa uzima, na wenye dhambi ufufuo wa hukumu.

viii. Kanisa la Yesu Kristo na umoja wa waamini.

ix.    Kuiweka imani ya kikristo kwenye utendaji wa maisha ya kila siku, na hitaji la kuwahudumia watu katika maeneo yote ya maisha  ambayo yanajumuisha siyo mambo ya kiroho tu, bali pia, kijamii, kisiasa na kimwili.      
                                                      
x.      Agizo kuu la Bwana Yesu, la kuipeleka injili kamili kwa ulimwengu wote linalojumuisha ubatizo wenye maji kwa kuzamisha na kuwafanya kuwa wanafunzi wa Yesu. Math 28:18-20.

8.0. UANACHAMA:

8.1.1.Mwanachama wa CPCT atakuwa dhehebu la kipentekoste litakalokubaliwa na wanachama na mamlaka iliyoidhinishwa na Katiba hii.

8.1.a.  Maneno “ Dhehebu la Kipentekoste” au “Dhehebu” katika Katiba hii yana maana ya shirika          lililosajiliwa kama kanisa kwa msajili wa vyama vya hiari na masharika yasiyo ya kiserikali, ambalo imani yake ya utendaji wake kwa mujibu wa tafsiri ya upentekoste na tamko la imani vilivyoainishwa kwenye Katiba hii, ni la kipentekoste.

8.1.b Huduma ya kipentekoste isiyo na makanisa inayosimamia, itaruhusiwa kuwa mshirika mwenza (associate member) lakini siyo mwanachama.

8.2 Sifa za uanachamaKila dhehebu linalokubaliana na kufuata tamko la imani ya CPCT na mafundisho ya kipentekoste 

8.3 Wajibu wa wanachama

8.3.1 Kulipa ada ya uanachama.

8.3.2 Kuhudhuria mikutano au vikao vilivyoainishwa na Katiba hii.

8.3.3 Kushiriki katika kutekeleza madhumuni ya CPCT

8.4 Haki za mwanachama zitajumuisha:

8.4.1 Haki za kupiga kura katika vikao na mikutano ya CPCT.

8.4.2 Haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi ndani ya CPCT

8.4.3 Haki ya kutoa mawazo kwenye mikutano halali na kusikilizwa.

8.4.4 Haki za kupewa huduma zote  kwa  mujibu miongozo itakayotawala utoaji wa huduma husika.

8.4.5 Wanachama shiriki wana haki zote isipokokuwa kupiga na kupigiwa kura.

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA (CPCT – MBULU)

Utaratibu  wa kujiunga na (CPCT – MBULU) utafafanuliwa  katika mwongozo.

8.5 Kuacha uanachama

8.5.1 Dhehebu -  mwanachama ataacha uanachama ikiwa litachagua lenyewe kufanya hivyo na kutoa taarifa kwa maandishi .

8.5.2  Dhehebu – Mwanachama litahesabiwa kuwa limepoteza uanachama ikiwa limethibitika kuwa limekengeuka kiimani, limevunja Katiba ya kanisa lake, limevunja katika ya CPCT limekiuka maadili ya msingi (core values) ya CPCT kama yalivyoinishwa katika vipengele 6.1. – 6.6

8.5.3  Iwapo Dhehebu – Mwanachama litakoma kuwepo / kuacha uanachama kwa sababu yoyote ile halitarudishiwa ada ya usajili, michango yoyote ya fedha au mali, na haki za uanachama. Pia halitakuwa na haki  ya kuidai  CPCT chochote.

8.5.4 Kutohudhuria vikao vitatu mfululizo  bila taarifa ya maandishi.

8.5.5 Kushindwa kulipa ada ya mwaka.

9.0 MUUNDO WA UONGOZI  NA MGAWANYO WA MADARAKA

9.1.1 Mkutano mkuu

9.1.2 Baraza la Waangalizi au washauri.

9.1.3 Kamati kuu ya utendaji

 9.1.4  Idara CPCT - MBULU

9.1.5 Kamati za Wilaya 

MKUTANO MKUU

9.2.1 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya watakuwa ni:

-a)      Wajumbe wote wa kamati wa utendaji wa Wilaya.

b)      Viongozi watatu wa ngazi  ya juu kutoka kila dhehebu mwanachama. 

c)       Wadhamini wote wa CPCT – MBULU

d)      Viongozi wa juu wawili wanachama shiriki kutoka kila kanda (associate members)

e)      Mwenyekiti na katibu wa  CPCT  kila Kanda.

f)       Wakurugenzi wa idara za CPCT  isipokuwa hawatakuwa na haki ya kupiga kura.

9.2.2 Majukumu ya mkutano mkuu yatakuwa haya

         i.            Kupokea na kujadili taarifa na mipango mbalimbali

       ii.            Kupokea wanachama wapya

iii.                    Kuwachagua, kuwatambua na kuwabariki viongozi wa Wilaya   

              waliochaguliwa na kuwapa  vyeti.

     iv.            Upitishaji bajeti ya kila mwaka.

 v.            Kuidhinisha idara mpya  za (CPCT – MBULU) zitakazoonekana zitahitajika.

     vi.            Kufanya maamuziya mwisho kuhusu mambo ya  ndani ya (CPCT – MBULU)

    vii.            Kuidhinisha marekebisho  ya katiba ya (CPCT – MBULU)

  viii.            Kuthibitisha  wadhamini

9.3. BARAZA LA WAANGALIZI NA WASHAURI (CPCT – MBULU) 

Baraza la Waangalizi na washauri watahudhuria mikutano mikuu yote. Baraza  hili litakutana  mara mbili kwa mwaka  au zaidi itokeapo mkutano mkuu.

Kutatua migogoro  ndani ya dhehebu  mwanachama inapokuwa mikubwa  na imeshindikana na kusuluhishwa ndani ya dhehebu husika.

9.3.1 Wajumbe wake ni hawa wafuatao 

i.         Mwenyekiti wa umoja wa wilaya (CPCT – MBULU)

ii.       Makamu mwenyekiti  (CPCT – MBULU)

iii.      Katibu mkuu wa Wilaya wa  (CPCT – MBULU)

iv.     Waangalizi na Wachungaji wa madhehebu  wanachama wa CPCT Wilaya.

9.3.2 mjumbe wa baraza  la  (CPCT – MBULU) atakoma kuwa mjumbe wa baraza hilo ikiwa ataacha uongozi (Uchungaji)  kwenye  dhehebu lake kwa sababu yoyote, au ikiwa dhehebu lake litafutiwa uanachama  wa  (CPCT – MBULU)  kwa mujibu wa katiba hii.

9.3.2 Majukumu ya baraza la Waangalizi 

i.         Kusimamia, kutetea, na kulinda imani ya kipentekoste Mbulu. 

ii.      Kupendekeza majina ya wadhamini wa CPCT

iii.     Kupitia ripoti  na mipango ya kamati ya utendaji  wa Wilaya kabla  ya kuwasilisha  
         kwenye mkutako mkuu

iv.       Kusimamia utekelezaji  wa maazimio ya mkutao mkuu.

v.     Kutoa misimamo ya pamoja  juu ya maswala ya kijamii Wilayani

vi.     Kuajiri/ kuwaachisha kazi katibu mkuu na msajili wa  wanachama wapya  
            watakaojiunga na Umoja wetu wa (CPCT – MBULU)  

vii.       Kuteua wajumbe wawili wa kamati ya utendaji 

xiii.     Baraaza hili litakutana mara mbili (2)  kwa mwaka au zaidi itakapohitajika.

ix.    Kupitisha miongozo mbalimbali ya idara

9.4 KAMATI YA UTENDAJI YA KIWILAYA

9.4.1 Kamati ya utendaji ya Wilaya itakutana mara nne kiwilaya kwa mwaka au zaidi itakapotokea dharura. Itaundwa na wajumbe wafuatao:-

i.         Mwenyekiti

ii.       Makamu mwenyekiti

iii.      Katibu mkuu

iv.     Wajumbe wawili na Mhasibu

9.4.2 Majukumu ya kamati ya Utendaji

i.         Kusimamia  utekelezaji   wa maazimio ya baraza la Washauri  na Waangalizi.

ii.       Kusimamia na kuratibu  vikao  vya Wilaya.

iii.      Kutayarisha taarifa ya mwaka kwa ajili ya Mkutano mkuu

iv.     Kusimamia mwenendo wa ofisi za (CPCT – MBULU) Wilaya

v.       Kusimamia utendaji wa idara za (CPCT – MBULU)

vi.     Kuandaa agenda za baraza la waangalizi na Mkutano mkuu

vii.    Kuratibu na kuwa msemaji kwa niaba ya baraza la wqaangalizi katika masuala ya uhusiano wa ndani na nje.

9.4. Majukumu Ya wajumbe  wa kamati ya utendaj (CPCT – MBULU)

9.4.1  Majukumu ya Mwenyekiti (CPCT – MBULU)

i.         Kuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya kamati kuu ya utendaji, baraza la   Waangalizi na mkutano mkuu (CPCT – MBULU).

ii.       Kuwa ndiye msemaji wa (CPCT – MBULU) katika mambo yatakayoamiriwa  na baraza la waangalizi, na mkutano mkuu.

9.4.2 majukumu ya makamu mwenyekiti

i.         Kukaimu kazi zote za mwenyekiti wakati mwenyekiti hayupo

ii.       Kufanya kazi zote anazoagizwa na mwenyekiti.

9.4.3 Majukumu ya katibu mkuu

i.         Kuratibu  uendeshaji na utunzaji wa kumbukumbu za mikutano yote ya kamati kuu ya utendaji, Baraza la Maaskofu, na mkutano mkuu

ii.       Atakuwa msimamizi mkuu wa ofisi kuu

iii.      Mtendaji wa kila siku wa shughuli za kamati kuu ya utendaji.

iv.     Kutunza haki zote muhimu za CPCT pamoja na muhuri wa moto (seal) wa CPCT.

v.       Kuratibu na kuungansha idara zote za CPCT

vi.     Kuwa mojawapo wa watia sahihi katika hundi zote za benki na mthibiti mkuu wa  
         fedha  watakaoajiriwa chini ya ofisi yake.

vii.    Katibu atapatikana kwa kupendekezwa  na kupigiwa kura na mkutano mkuu na
           atafanya kazi kwa mkataba wa miakaka mitatu.

9.4.7 Sifa za katibu

i.         Awe mtumishi wa injili aliye na uzoefu wa huduma  isiopungua miaka mitano
           katika mji wa Mbulu

ii.       Awe na elimu ya darasa la saba na kuendelea.

iii.      Awe mwadiliifu, asiwe na kashfa machoni mwa jamii.

iv.     Awe na uwezo wa kuwasiliana 

9.4.9 Muda wa kutumika kwa mjumbe wa kamati ya utendaji

Viongozi hawa watakuwa katika wadhifu huo kwa muda wa miaka mitatu.Waweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha pili nafasi ya mwenyekiti itakuwa yamzunguko kwa muda wa miaka mitatu kwa kila dhehebu mwanachama.

9.4.10. TARATIBU ZA KUENDESHA VIKAO

i.         Vikao vyote vya (CPCT) vitafanyika kwa namna ambavyo imeelezwa nadani ya katiba  ya CPCT. Kikao ambacho hakitafuata utaratibu uliotajwa ndani ya katiba  ya CPCT kitakuwa batili.

ii.       Vikao halali vya CPCT vitakuwa na wajumbe  wasiopungua theluthi mbili (2/3)  ya wajumbe wa ngazi husika  (kwa kikao chochote  ndani ya  CPCT)

iii.      Maamuzi ya vikao  vyote vya CPCT vitakuwa ni theluthi mbili (2/3) ya wajumbe wa mkutano husika.

10.0 SIFA ZA VIONGOZI

Kukubaliana na sifa zote  za kibiblia na kuwa :-

10.1 Mtu ambaye amezaliwa mara ya pili

10.2 Mtu abaye amejazwa roho mtakatifu 

10.3 Mume wa mke  mmoja 

10.4 Mwenye vipawa na uwezo wa uongozi 

10.5 Ni lazima awe na ushuhuda mzuri  

10.6  Mtu mwenye elimu ya kusoma na kuandika

10.7 Awe na uwezo  wa kuwasiliana 

11.0. JINSI YA KUWAPATA VIONGOZI WA  CPCT

11.1 Viongozi wa CPCT watapatikana kutokana na uchaguzi utakaofanyika katika mkutano mkuu wa mwaka  wa uchaguzi, kila baada ya miaaka miatatu. Mwenyekiti na makamu mwenyekiti  wa CPCT taifa watachaguliwa katika mkutano mkuu  wa uchaguzi  kutoka miongoni mwa viongozi wachungaji wa dhehebu na wanachama kwa ajili ya kupigiwa kura. 

11.2 Viongozi watachaguliwa kila wiki ya wiki ya kwanza ya mwezi wa sita mwaka  wa uchaguzi. Makabidhiano  ya kiofisi yatafanyika ndani ya siku thelathini (30) baada ya uchaguzi.

11.3 Wiongozi waliochaguliwa watakauwa madarakani kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane ya mwaka wa uchaguzi hadi tarehe 30 mwezi wa saba ya mwaka mwingine wa uchaguzi

11.4 Wakati wa uchaguzi wa kiwilaya, koramu ya wajumbe lazima ifikie ziada ya asilimia hamsini ya wanachama hai (kwa kulipa ada) zote na mchango kwa bajeti ya CPCT  Wilaya) na pia kigezo cha aliyechaguliwa kitakuwa ni theluthi mbili ya kuwapiga kura iwe ya siri kwa wote.

11.5 utratibu huu utatumika kwa chaguzi za kamati ya utendaji Wilaya, tarafa na kata.

12.0 KUACHA UONGOZI

 Kiongozi yeyote wa CPCT itambidi aache uongozi kkufuatia mojawapo  ya hali hizi zifuatazo  ikitokea:

12.1 kumalizika kwa muda wa kushika uongozi 

12.2 kuacha uongozi kwa hiari ya kiongozi mwenyewe akiwa ametoa taarifa ya miezi mitatu kwa maandishi kuhusu jambo hilo  kwa mamlaka iliyomchagua ya CPCT

12.3 Wakati ule atakapoacha kuwa mwakilishi wa dhehebu lake.

12.4 Wakati atakapothibitishwa na Baraza la waangalizi kwamba amekiuka katiba na tamko la imani ya  CPCT

12.5 Atakapokuwa ameshindwa kuhudhuria vikao vya kawaida vya  CPCT vitatu mfululizo bila ya kuwa na sababu za maana  zenye kuridhisha.

13.0 IDARA ZA CPCT - MBULU

Baraza la maaskofu baada ya ushauri wa kamati ya utendaji kubadilika itaanzisha idara yeyote ile kwa kusudi la kurahisisha  utendaji wa kazi  za CPCT kama ifuatavyo;

a)      Uinjilisti na umisheni

b)      Idara ya thiologia

c)       Mambo ya kimataifa na mahusiano (Mf. compassion, world vision nk)
 
d)      Habari za utangazaji na uchapaji (Mfano kutoa habari za umoja wetu kwenye
         magazeti, blogs, mahojiano ya Radio, kotoa vijarida vinavyoelezea maendeleo
         au mafanikio ya umoja huu, Television nk

e)      Fedha uchumi, na mipango

f)       Huduma za jamii na miradi ya maendeleo

g)      Idara za vijana (mashuleni, vyouni, na vyuo vikuu)

h)      Idara ya wanawake 

i)        Idara ya elimu na mafunzo 

(Mfano kuandaa semina mbalimbali au kuwatoa baadhi ya wajumbe kwenye umoja wetu kwenda kuwasomesha kwa ajili ya kuendesha miradi mipya ambayo itatokana na umoja wetu).

13.1 IDARA YA UINJILISTI NA UMISHENI

14.1 idara hii itakuwepo kwa kusaidia na kuratibu na kusimamia upelekaji wa innjili kwa njia ya mikutano mikubwa ya hadhara, kubuni na kuhamasisha mbinu mbalimbali za uinjilisti wa ushirikiano wa madhehebu  wanachama. Pia itaratibu na kushauri juhudi za dhehebu lolote  mwanachama lililo na mipango ya kufanya umisheni ndani na nje ya nchi ikiwa n pamoja na kulitafutia vitendea kazi kwa bei nafuu.

14.2 Viongozi wa idara hii watakuwa:-

Mkurungenzi mkuu atakayekuwa mwenyekiti wa vikao vyote na kiongozi mkuu.

14.3 naibu mkurungenzi mkuu atakayemsaidia mwenyekiti katika shughuli zake na kukaimu uenyekiti anapokuwa hayupo.

14.4 Katibu ndiye atakayekuwa mtendaji mkuu wa maamuzi yote ya kamati, na wajumbe wanne.
14.5 sifa za viongozi zitakuwa Kama ifuatavyo:-

i.         Mwenyekiti awe mtumishi wa injili mwenye uzoefu wa kuratibu mikutano  mikubwa ya injili  kwa muda usiopungua miaka mitano.

ii.      Atokane na moja ya dhehebu mwanachama.

Wajumbe wanaweza kuwa washiriki au watumishi wa madhehebu wanachama wanaojulikana kuwa na uzoefu katika huduma ya uinjilisti, mwenye mzigo na uzoefu wa mikutano ya injili.

13.2  IDARA YA THEOLOJIA 

13.1 Idara hii itakuwepo na makusudi ya kulinda imani na kuitetea dhidi ya upotofu unaweza kuathiri au kutoa taswira mbaya  ya upentekoste, kubuni, kuraitibu na kuwezesha utoaji elimu ya biblia na theologia  yenye malengo au mkazo wa kipentekoste, na kutoa mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuharakishwa utimizaji wa malengo ya CPCT. Idara hii itaratibu na kuandaa makongamano ya kiwilaya na kitaifa ya mafundisho ya kiroho na uamsho ya kipentekeste yatakayoshirikisha madhehebu wanachama wote.

13.2 Vongozi wa idara hii watakuwa:-

i.         Mkurugenzi mkuu ambaya atakuwa mwenyekiti na kiongozi mkuu

ii.       Naibu mkurungezi mkuu atakayemsaidia mwenyekiti

iii.      Katibu mkuu atakayekuwa mtendaji mkuu wa maamuzi ya kamati, na wajumbe watano kutoka kwenye madhebu wanachama. Mkurungezi mkuu atatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

-          Awe mtumishi wa injili mwenye uzoefu katika huduma usiopugua miaka kumi.

-          Awe na uwezo wa kufundisha, kutetea na kujenga hoja.

-          Awe madilifu, asiye na kashfa mbele ya jamii

Naibu wake, na katibu watakuwa na sifa zifuatazo:-

Wawe na elimu au zaidi pamoja na sifa nyingine kama za mkurungenzi mkuu. Wajumbe wengine wa kamati  wawe watumishi wenye uzoefu katika huduma ya injili isiopungua miaka mitano.

13.3. IDARA YA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO

 Majukumu yake yatamjulisha:-

i.         Kuratibu maandalizii na uundaji wa sera na mipango mikakati ya CPCT ikishirikiana na baraza la waangalizi/washauri
ii.       Kukagua na kutolea taarifa  na ushauri utekelezaji wa sere na mipangoo mikakati, mipango maalum kwa baraza la waangalizi/washauri.

iii.      Kushauri baraza la waangalizi na idara nyingine za CPCT katika masuala ya kiushumi na uandaaji bajeti zake.

iv.     Kutoa ushauri kwa wanachama wa CPCT katka mambo yahusuyo mipambo, na maendeleo yafaayo wakati utakapohitajika.

13.3.1 Idara hii itaundwa na bodi yenye wajumbe wafuatao:-    

i.         Mkurugenzi mkuu. Huyu atakuwa mwenyekiti wa mikutano yote ya bodi, na kiungo katika bodi ya baraza la waangalizi

ii.       Makamu mwenyekiti. Huyu atakuwa mshauri wa mwenyekiti na kufanya kazi zake anapokuwa hayupo na amekasimu madaraka kwa makamu.

iii.      Mratibu mkuu. Atachukua na kutunza miniti za vikao vya bodi, na msimamizi mkuu wa vitengo vya bodi.

 13.3.2 Bodi itakuwa na vitengo vivuatavyo:-
      Kitengo mpango mkakati;    Kitengo hiki kitahusika na uandaaji  wa mpango mkakati na usimamizi wa mchakato wake wote. Kitaundwa na wajumbe kumi  wenye taaluma ya mipango. Katika wajumbe hao kumi watatu lazima wawe wachungaji.

Sifa za wajumbe hao ni:-

i.         Wawe washirika au wachungaji watokanao na madhehebu wanachama

ii.       Wawe na stashahada ya kwanza au zaidi ya mipango mingine yoyote inayojumuisha elimu  ya mipango na utawala.

13.3.3  Kitengo cha uchumi na fedha

Kitengo hiki kitahusika  mipango  ya mambo ya uchumi, upatikanaji na uwezeshaji mali na fedha , na usimamizi au ukaguzi wa mahesabu (accounting and auditing) na maandalizi ya bajeti  ya baraza la waangalizi la CPCT ya mara kwa mara. Kitengo hiki kitaundwa na wataalum wafuatao wa fedha:-

i.         Mkurugenzi makamu wake utawala (managing  director) atakayesimamia vikao na utendaji wa kitengo

ii.       Mtunza mahesabu mkuu (chief accountant ) atakayesimamia timu ya utawala wa mwendo wa mahesabu ya fedha CPCT.

iii.      Mtunza maahesabu utawala  (management accountant) atakayesimamia na kutoa taarifa ya halali ya fedha kwa utawala wa ndani (management accounting) wa CPCT 

Hawa, pamoja na kazi nyingine watakazofanya kulingana na majukumu yao kama yalivyoaininshwa hapo juu, watakuwa na vikao vya pamoja vitakavyoandaa mipango ya uchumi na bajeti za CPCT  kwa kuzingatia taratibu rejea zitakazoagizwa na baraza la wangalizi kwa marrekebisho/maridhio.

13.4 IDARA ZA HUDUMA ZA JAMII NA MIRADI YA MAENDELEO 

Idara hii itakuwepo kwa kusudi la kubuni na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na maafa  kama elimu, Afya   huduma za kifedha, ufundi stadi, biashara, utoaji misaada kwa waliopata majanga ya mafuriko, moto au mengineyo, idara hii pia itashirikiana na idara ya utendaji  ya CPCT  itatafuta fedha nje na ndani ya nchi kwa kusudi lakufikia malengo yake 

13.5. IDARA YA ELIMU NA MAFUNZO 

Majukumu yake yatajumuisha

i.         Kuchambua kwa kina na kuwezesha kupata nafasi za mafunzo kwaajili ya watumishi wa Mungu walio  chini ya wanachama wa CPCT

ii.       Kupanga kuendsha na kuunganisha mambo yahusuyo mafunzo ya muda mfupi  na semina hapa nchini

iii.      Kuchambua kwa makini watoa misaada na kuwatuma watumishi wa mungu  na wakristo nchi za nje wapate mafunzo

iv.     Kuanzisha mashule,  vyuo na vyuo vikuu kwa ajili ya  kufundisha  wakristo na watumishi wa Mungu

v.       Atawajibika kwa Katibu Mkuu

13.6. IDARA YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

13.6.1 Idara hii itakuwepo  kwa kusudi la kuratibu upelekaji wa huduma za kiroho kwa wanafunzi katika shule za msingi, na sekondari kwa watoto watokao kwenye makanisa ya kipentekoste. Kwa kuunganisha juhudi za pamoja za madhehebu wanachama, idara hii itaratibu utoaji wa mafundisho na huduma kwa wanafunzi wilaya yote.

13.6.2 Viongozi wa idara hii watakuwa ni:

i.         Mkurugenzi mkuu atakayekuwa mwenyekiti na kiongozi mkuu wa idara.

ii.       Naibu mkuruugenzi mkuu atakayemsaidia mwenyekiti  

iii.      Katibu mkuu atakayekuwa mtendaji mkuu wa maamuzi ya uongozi.

13.6.3 Sifa za viongozi hawa zitakuwa kama ifuatavyo:-

i.       Atakuwa mtumishi wa injili mwenye wito na wanafunzi ili atoe muda kwa kazi hiyo.

ii.       Awe na elimu ya theologian a kutumikia miaka zaidi ya tano 

iii.      Asiwe na kashfa machoni pa jamii

13.6.4 Makamu mkurugenzi – awe na sifa zote za mkurugenzi mkuu. Katibu mkuu awe na sifa 
           za mkurugenzi mkuu isipokuwa halazimiki 

13.7 IDARA YA WANAFUNZI WA VYUO NA VYUO VIKUU

i.         Idara hii itakuwepo kwa kusudi la kuratibu utoaji huduma za kiroho kwa wanafunzi wa vyuo vikuu watkao kwenyye makanisa ya kipentekoste nchini  

i.       Viongozi  wa idara hii watakuwa na sifa kama viongozi wa idara ya viongozi wa idara ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ispokuwa sifa ya elimu za viongozi. Viongozi wa idara hii watapaswa kuwa na elimu ya theolojia ya shahada moja au nyingine 

iii.      Idara hii itakuwa na mwongozo wake utakao fafanua utendaji kazi wake.

14.0 WAWAKILISHI WA CPCT WA MKOA, WILAYA, TARAFA AU KATA

14.1 kutakuwepo na wawakilishi wa CPCT kayika mikoa na wilaya za Tanzania. Chaguzi la wawakilishi wa CPCT ngazi ya mkoa na wilaya zitafanyika mwezi wa tisa baada ya viongozi wapya kuingia madarakani.

14.2. utaratibu wa kuundwa kwa ofisi za mikoa na wilaya kutafafanuliwa  katika  mwongozo wa utendaji ambao  utaandaliwa kuwa mujibu wa katiba hii.

14.3 sifa za wawakilishi, muda wao wa kushika nafasi hizo na kuacha kazi kwao vitakuwa sawa na ilivyo kwa ajili ya nafasi nyingiinezo za uongozi ndani CPCT

15.0 WADHAMINI WA MALI ZA CPCT 

15.1 wadhamini

15.2. CPCT itakuwa na wadhamini saba watakaosajiliwa kisheria.

15.3. wadhamini hao watajumuisha watu saba wafuatao:-

i.         Mwenyekiti wa CPCT 

ii.       Katibu mkuu wa CPCT 

iii.      Wajumbe watano watakaokuwa mamechaguliwa miongom=ni mwa baraza la waangalizi

15.3.1 wadhamini watamchagua mwenyekiti wao ambaye ndiiye atakuwa mdhamini mtendaji na mtunza mihuri

15.3.2 wadhamini watawajibika kutunza mali zote  za CPCT zinazohamishika zikijumlishwa na ardhi  na vilivyo ndani yake, majengo, mashine, magari na mali yoyoite ile ambayo inapatikana kwa jina la CPCT.

15.3.3 wadhamini watashika wadhifa huo kwa miaka mitatu mfululizo lakini waweza kuchaguliwa kwa muda wa miaka mitatu mingine.

15.3.4 mdhamini yeyote ataacha kuwa mdhamini kwa:-

i.         Mda wa wadhifa wake utakapoisha

ii.       Yeye mwenyewe kwa hiari yake  kutoa taarifa mapema kwa mkutano mradi tu awe hana deni na CPCT                                                                                                          

 iii.      Sababu kuna ushahidi wa kuaminika kwamba mdhamini Yule ni mbinafsi na kwamba ametumia mali ya CPCT kwa faida yake binafsi.

iv.     Dhehebu atokalo likikoma uanachama

v.       Uongozi wake ukikoma katika dhehebu lake

vi.     Akifariki

16.0 MIHURI

Kutakuwa na mihuri ya aina mbili

i.         Mhuri wa chuma   

ii.       Mhuri wa kawaida

Wadhamini watautunza mhuri wa CPCT mahali pa usalama na kuhakikisha kuwa unatumika  kihalali. Uwekaji wa mhuri wa CPCT katika hati yoyote itabidi ufanywe na wadhamini wa CPCT  wasiopungua watatu, mmojawapo lazima awe mwenyekiti au katibu mkuu au mmoja wa wadhamini.

17.0 MALI YA CPCT.

17.1 CPCT  MBULU itajipatia mali yake yenyewe na kuimiliki kwa kuipata katika sehemu yeyote nchini au nje ya Tanzania kwa ajili ya matumizi yake  na itahiari kuiondoa mali yake baada ya kupata kibali cha mkutano mkuu   wa CPCT

17.2 mali yote Ya CPCT  itatunzwa na kutawaliwa  na wadhamini ambao watakuwa wamechaguliwa na chombo kinachohusika  cha CPCT 

17.3 Mwanachama yayote wa CPCT  ambaye ataacha kuwa mwanachama kwa sababu  iwayo yoyote ili hatadai kulipwa sehemu yoyote ya mali ya CPCT 

18.0 USHAURI WA KISHERIA

CPCT itatafuta ushauri  wa kisheria, katika mambo ya mikataba, matamko na mambo mbalimbali yahusuyo sheria.

19.0 USHIRIKIANO

CPCT – MBULU inatambua na itajiunga na mashirika mengine ya kipentekoste ya Wilaya na kitaifa kwa kusudi la kujenga ushirika wa kiroho, na kuunganisha nguvu za kihuduma kwa kuanzia hapa inatamkwa wazi kuwa CPCT itajiunga rasmi kuwa mwanachama wa pentekoste world fellowship (PWF) ambalo tamko lake la imani imekubali kuwa tamko lake pia.

20.0. MIONGOZO MBALIMBALI YA UTENDAJI

20.1 kwa mujibu wa katiba hii, pia kutakuwepo na miongozo ya utendaji ambayo itaweka utaratibu na kanuni mbalimbali zitakazosaidia kuendesha  CPCT ili mradi miongozo hiyo haikiuki sheria zilizomo ndani ya katiba hii.                                                                       

20.2 Ni lazima miongozo yote iwe na sahihi ya mwenyekiti wa baraza la waangalizi na katibu.

20.3 kila idara itaundwa mwongozo wa idara yake utakapopitishwa na baraza la Waangalizi ikishirikiana na wataalum wa mambo ya sheria.

21.0 MAREKEBISHO YA KATIBA YA CPCT

Mkutano mkuu unaweza kurekebisha katiba mradi:

21.1 taarifa ya maandishi ya miezi mine kabla ya mkutano mkuu iwe imetolewa na mwanachama yeyote kwa katibu mkuu kabla ya kikao cha mkutano mkuu akionyesha kusudi lake la kutaka katiba  irekebishwe atajaza wap na kifungu kipi na vifungu vipi virekebishwe an kwa sababu zipi  anapendekeza marekebisho.

21.2 kamati kuu itatoa maandishi  miezi miwili kwa wanachama wa CPCT  kabla mkutano mkuu haujakaa ikionyesha kusudi la kurekebisha katiba kwa kuta wazi ni kifungu  au vifungu vipi inapendekeza virekebishe
21.3. Mkutano mkuu utakaorekebisha katiba utahitaji kuhudhuriwa na 50% ya wanachama wote wa CPCT na katika   hao watakaohudhuria wawe wamepiga kura  ya kukubali mapendekezo ya kirekebisha katiba.
Imetolewa na :
Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT – Mbulu), Manyara, Tanzania au
Council of Pentecostal Churches of Mbulu in Tanzania (CPCT)
22.0 ANUANI, EMAIL NA BLOG YA BARAZA LA WAANGALIZI LA 
UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE MBULU

SLP 103, MBULU, MANAYARA – TANZANIA
Simu / +255 784 890 972; +255 784 478 177,
Blog ya umoja wa CPCT Mbulu;  cpctmbulu.blogspot.com